Tatizo hili husababishwa na kuzidi kwa homoni ya maziwa inayojulikana kama Prolactin hormone. Homoni hii huwa inakuwepo kwa jinsia zote mbili ila hutofautiana kwa viwango tu kwa mwanaume huwa ipo chini zaidi na mwanamke ambaye sio mjamzito huwa ipo kwa wastani, na kwa mwanamke ambaye ana mimba au ananyonyesha huwa ipo juu zaidi na zaidi.
Sasa kuna baadhi ya wanawake homoni hii huwa juu sana kiasi cha kusababisha maziwa kutoka wakati hana mimba na wala hanyonyeshi hapa sasa ndio tatizo lilipo. Napenda ufahamu kuwa ikiwa mwanamke anakabiliwa na tatizo hili ni vigumu sana kwake kushika mimba. Hivyo ikiwa una tatizo hili na unatamani kushika mimba basi anza kwanza kujitibia tatizo hili ndio ufikiriwe kuhusu kubeba mimba. Njia rahisi ya kukusaidia kujitibia tatizo hii ni kwa kujifukiza majani yaitwayo fwefwe. Unatumia mbelewele za majani hayo, chukua kiasi kidogo na uzichome kwenye moto na ujifukize kwenye maziwa yako fanya zoezi hili kwa siku saba mfululizo.
Unaweza kutazama video hapo chini uweze kufahamu vizuri Majani hayo