Dawa ya U.T.I sugu

Neno U.T.I ni kufupisho cha maneno Urinary Tract Infections ikiwa na maana maambukizi kwenye njia ya mkojo na mfumo wake. U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bacteria waitwao Escherichia coli (E. Coli) ambao huingia mwilini na kwenda kuathiri mfumo wa mkojo. Wanawake ndio wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu kuliko wanaume kutokana na sababu za kimaumbile. Ikiwa umepimwa na kuambi- wa kuwa una tatizo hili basi tumia dawa hii;

Mahitaji:

(i.) Vitunguu maji vikubwa vinne(4)

(ii.) Baking soda (Bicarbonate)

(iii.)Maji lita moja na nusu

Matayarisho na matumizi yake:

Katakata vitunguu vyako na uvichemshe kwenye maji lita moja na nusu kwa dakika kumi (10), epua na acha yapoe ukiwa umefunika sufuria yako. Baada ya kupoa yachuje na uhifadhi kwenye chombo safi chenye mfuniko.

Chukua kikombe cha maji ya vitunguu kisha weka nusu kijiko cha chai cha baking soda na ukoroge vizuri. Mgonjwa anywe kikombe kimoja asubuhi na kingine jioni kwa siku 3 mfululizo kwa uwezo wa Mungu atakuwa amepona kabisa. Pia unaweza kuepukana na tatizo hili kwa kunywa maji mengi, kuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango, kula vyakula vya asili, kukojoa mara baada ya kushiriki tendo la ndoa, kujitahidi kuwa msafi nyakati zote na kuacha matumizi ya pombe na sigara.

About the author

Topten Herbs

Topten Herbs ni kituo cha utafiti wa Tiba mbadala zinazoweza kusaidia jamii yetu kujitibia maradhi mbalimbali yanayotukabili kirahisi kabisa kwa kutumia vitu mbalimbali vinavyotuzunguka katika mazingira yetu. Kituo hiki kinapatikana Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

View all posts

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *