Dawa ya Kifua

Mahitaji:

(i.) Asali kikombe robo lita (250mls

) (ii.) Vitunguu maji vikubwa Vitatu

Matayarisho na matumizi yake:

Saga vitunguu vyako viwe kama uji kisha changanya na asali yako

Kwa Mtu Mzima: Kula vijiko viwili vya chakula kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi 5

Kwa mtoto: Kula kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara mbili kwa siku 3 hadi 5.

Ikiwa huwa hutumii asali basi unaweza kutumia unaweza kuchemsha majani ya mkaratusi na unywe maji yake nusu kikombe kutwa mara 3 kwa siku 3. Ikiwa sehemu ulipo hakuna majani ya mkaratusi unaweza kutumia majani ya mbaazi au majani ya mkorosho kujitibia tatizo hilo za Kifua.

Ikiwa kifua hicho kinamsumbua mtoto wa chini ya mwaka mmoja basi au mtu yeyote ambaye hawezi kutumia asali basi yeye unatakiwa kumtengenezea dawa ifuatayo.

Mahitaji:

Kitunguu Maji

Sukari

Matayarisho na matumizi yake:

Katakata kitunguu chako vipande vidogovidogo kisha weka sukari vijiko viwili vikubwa vya sukari. Koroga vizuri mchanganyiko huo kisha hifadhi kwenye kopo lenye mfuniko kwa masaa sita. Baada ya muda huo utaona ile sukari yote imeyeyuka na kuwa maji kabisa Chukua kijiko kidogo kimoja cha hayo maji mpe mtoto mwenye shida hiyo ya kifua kwa siku mara 3 kwa siku tatu hadi tano kwa uwezo wa Mungu atakuwa amepona kabisa. Dawa hii inaweza kutumika kwa mtu mzima pia ila yeye atumie vijiko vikubwa vitatu kutwa mara 3 kwa siku 3 hadi 5.

About the author

Topten Herbs

Topten Herbs ni kituo cha utafiti wa Tiba mbadala zinazoweza kusaidia jamii yetu kujitibia maradhi mbalimbali yanayotukabili kirahisi kabisa kwa kutumia vitu mbalimbali vinavyotuzunguka katika mazingira yetu. Kituo hiki kinapatikana Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

View all posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *