Dawa ya Bawasiri

Je, Unajua Bawasiri/Hemorrhoids Ni Nini?

Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS na kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles.

Tatizo la bawasiri huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50.

Nini Chanzo Cha Bawasiri?

Bawasiri kwa kiasi kikubwa huletekezwa na kuongezeka kwa mgandamizi ama presha mara nyingi ni pale unapojikaza ili kutoa haja kubwa. Hivo bawasiri huwatokea zaidi watu wenye matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji mfano unapata choo kigumu, tumbo kujaa gesi, kukosa choo kwa siku kadhaa. Wanawake wenye ujauzito pia huwa kwenye hatari kubwa ya kupata bawasiri kutokana na mtoto aliye tumboni kugandamiza tumbo la chakula na hivo kuathiri utoaji wa haja kubwa, kwa bahati nzuri bawasiri yanayosababishwa na ujauzito huanza kuisha pale tu mama anapojifungua. Watu wenye kitambi na uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasiri kutokana na mwili kushindwa kutengeneza nishati ya kutosha kusukuma uchafu kwenye utumbo.

Mahitaji:

(i.) Unga wa magome ya mng’ongo vijiko vya chakula vinne( 4)

(ii.) Unga wa habat soda vijiko vya chakula vinne( 4)

(iii.) Bakali hadi vijiko vya chakula vinne( 4)

(iv.) Manemane vijiko vya chakula vinne( 4)

(v.) Mafuta ya nyonyo

Matayarisho na matumizi yake:

Changanya mng’ongo, habbat soda, bakali hadi, na Manemane kisha chemsha kwenye maji ya lita sita, viache vichemke kwenye moto wa wastani kwa dakika 20 hadi 30, epua na uache ipoe ikiwa imefunikwa. Baada ya kupoa chuja kwa chujio au kitambaa safi upate maji yake tu.

Mgonjwa anatakiwa kunywa nusu kikombe cha dawa hii kutwa mara mbili kwa siku 25, Pia mgonjwa anatakiwa kuwa anapaka mafuta ya nyonyo kwenye huo uvimbe wa bawasiri kila anapotoka chooni. Pia ni muhimu sana kuzingatia utaratibu wa kula kama nilivyoelekeza kwenye sura ya kwanza ya kitabu hiki.

slot 4d

About the author

Topten Herbs

Topten Herbs ni kituo cha utafiti wa Tiba mbadala zinazoweza kusaidia jamii yetu kujitibia maradhi mbalimbali yanayotukabili kirahisi kabisa kwa kutumia vitu mbalimbali vinavyotuzunguka katika mazingira yetu. Kituo hiki kinapatikana Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

View all posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *