Minyoo huishi ndani ya matumbo yetu, na inakadiriwa kuwa karibu 25% ya watu wote duniani wanakabiliwa na tatizo na maambukizi hutokea kwa njia ya kula chakula kilichoathiriwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo aina ya askaris. Mara nyingi dalili zake ni homa, kuvimba, kuhara, mtoto kudumaa, mengine mengi. Ili uweze ku- jitibia tatizo hilo fanya hivi.
Mahitaji:
Mbegu za papai zilikomaa vizuri
Matayarisho na matumizi yake:
Chukua mbegu zilizokomaa vizuri zikaushe kisha zisage upate unga wake.
Chukua kijiko kimoja kidogo cha unga wa mbegu za papai weka kwenye maji nusu kikombe cha chai koroga vizuri na unywe kila siku asubuhi kabla ya kula kwa siku tano mfululizo.