Vidonda vya tumbo ni miongoni mwa magonjwa ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili wa binadamu. Hivi ni vidonda ambavyo vinapatikana ndani ya tumbo la binadamu na huwapata sanasana watu wazima kuliko watoto wadogo. Mara nyingi tatizo hili husababishwa na kutokula kwa wakati unaostahili na msongo wa mawazo. Sasa ili kuweza kujitibia tatizo hili ukiwa nyumbani unahitaji kuandaa
Mahitaji:
- Unga wa manjano
- Asali
Matayarisho na matumizi yake:
Chukua maji ya vuguvugu kikombe kimoja cha chai kisha chukua kijiko cha chai cha unga wa manjano weka kwenye maji hayo na ukoroge vizuri kisha weka kijiko kimoja kikubwa cha asali kwenye mchanganyiko wako huo koroga tena na mgonjwa anywe kikombe kimoja asubuhi, kingine mchana na kingine jioni. Tumia dawa hii kwa wiki tatu hadi mwezi kwa uwezo wa Mungu utakuwa umepona.