Napenda nianze kwa kukupa pole wewe unae amini kuwa presha ni ugonjwa pole sana, maana kufikiria hivo tu ndio ugonjwa wenyewe. Hebu turudi nyuma kidogo, ikiwa una mgonjwa ambae haongei wala hawezi kufanya kitu chochote njia pekee ya kuangalia kuwa bado yupo hai ni kutazama tu mapigo yake ya moyo. Ikiwa moyo bado unafanya kazi ndio huwa tunasema mgonjwa wetu bado yu hai. Kumbe mapigo ya moyo ni uthibitisho kuwa tupo hai.
Sasa mapigo ya moyo yanaweza kubadilika kulingana na hali tuliyopo, kwa mfano ukiwa umekaa mapigo ya moyo yanaweza kuwa ya kawaida na ghafla kikitokea kitu cha kukushtua mapigo ya moyo yatabadilika, ni jambo la kawaida tu hili. Ikiwa utapimwa presha kabla ya kuanza mashindano ya kukimbia na ukapimwa baada ya kumaliza mashindano majibu ya kule unakomalizia yatakuwa juu kuliko yale ya kabla hujaanza mashindano. Nafikiri sasa unapata kuelewa kidogo kuhusu presha.
Acha nikupe mfano mwingine nafikiri umewahi kuona maji yakitoka kwenye bomba, ikiwa maji yatakuwa mengi zaidi na bomba ni jembamba sana basi presha ya maji huwa kubwa na kinyume chake kuwa kama maji ni kidogo na bomba ni kubwa basi presha huwa ndogo ni mambo ya kawaida sana haya.
Ndivyo ilivyo na kwenye mwili wetu ikiwa damu ni nyingi sana na mishipa ya damu itakuwa myembamba sana kwa sababu ya mafuta mengi lazima tutapata na tatizo la presha ya juu na ikiwa damu itakuwa kidogo na mishipa ni mipana sana tutapata tatizo la presha ya chini. Nafikiri tumeelewana hapo, acha kudanganywa kuwa presha ni ugonjwa, na usitegee presha itatulia kama maji mtungini presha inabadilika kulingana na mazingira tuliyopo, hali ya afya yetu, na sababu nyingine nyingi.
Nafikiri sasa kichwani utakuwa unajiuliza ikiwa presha sio ugonjwa inakuwaje watu wanaambiwa kuwa wanatatizo na wanameza dawa kila siku? Napenda leo ufahamu kuwa zile dawa anazopewa mtu kwa ajili ya presha sio tiba ila ni blood thinner ni kitu ambacho husaidia kuifanya damu iwe nyepesi zaidi na iweze kufika sehemu mbalimbali za mwili kwa uharaka. Ndio maana unatakiwa kuzimeza kila siku, maisha yako yote kwa sababu sio tiba. Hebu shtuka unageuzwa mtumwa kidigitali, badala ya kutumia hela zako kununua dawa ambazo hazitibu tatizo basi anza leo kufuata utaratibu wa kula niliokufundisha kwenye sura ya kwanza ya kitabu hiki na utakuwa huru kabisa kutoka kwenye mtego huu wa watoto wa mjini wanaotaka uwe mteja wa dawa zao kwa maisha yako yote. Ukianza tu kufuata utaratibu huo acha pia kumzea dawa hizo na hakika mwenyewe utashamgaa jinsi maisha yatakavokuwa safi na mazuri. Ikiwa umekuwa na tatizo hili kwa muda mrefu sana basi tumia dawa hii.
Mahitaji:
(i.) Kitunguu maji chekundu
(ii.) Tangawizi mbichi
(iii.) Manjano mbichi
(iv.) Asali Mbichi
Matayarisho na matumizi yake:
Saga vitu vyote kisha uchanganye na asali na mgonjwa ale vijiko vikubwa viwili vya dawa hiyo kutwa mara 2 kwa siku 10 na huku anatakiwa kufuata utaratibu wa kula ataona kila kitu kimekaa sawa kabisa. Watu wengi wanaosumbuliwa na tatizo hili za presha ni wale wenye uzito uliopitiliza, sasa ikiwa na wewe ni mmoja wao basi pambana kupunguza uzito wako. ukifanikiwa kupunguza uzito wako na presha itakaa sawa yenyewe bila kutumia dawa yoyote.
Ikiwa unatamani kupunguza uzito na hujui utafanyaje basi Soma hapa DAWA YA KUONDOA KITAMBI HARAKA
Nimependa maelezo yako ya kina na kisayansi kabisa.
Nitakutembelea
Ahsante sana kwa kutenga muda wako kusoma makala zetu