Dawa rahisi ya Chango

CHANGO la uzazi ni miongoni mwa magonjwa yanayoshambulia viungo vya uzazi vya mwanamke ambapo humsababishia maumivu makali ya tumbo na kushindwa kupata ujauzito, au mimba kuharibika kila zinapoingia.

Zipo aina nyingi za chango ambazo zinaweza kujitokeza kila moja peke yake au zikajikusanya na kujitokeza kwa pamoja, mkusanyiko huu ndiyo unaitwa Ovulation Disorder (O.D).

Chanzo Cha Tatizo

Matatizo ya chango la uzazi, inatokana na vifuko vya mayai ya uzazi (ovaries) kutokuwa na uwezo wa kuzalisha mayai na kufanya yakue kwa wakati muafaka. Mwanamke mwenye matatizo haya hushindwa kuwa na siku za hatari za kunasa ujauzito na kama zipo basi huwa hazina mpangilio unaoeleweka.

Yawezekana mwanamke mwenye tatizo hili akawa na uwezo wa kuzalisha mayai lakini yakashindwa kukomaa au hata yakikomaa yakashindwa kusafiri kwenye mirija ya uzazi kwenda kukutana na mbegu za uzazi za kiume kwa ajili ya kurutubishwa.

Mahitaji:

Majani ya mzugwa/mvuga

Matayarisho na matumizi yake:

Chukua majani ya mvuga au mzungwa chemsha kwa dakika 10 acha yapoe kisha chuja.

Mgonjwa anatakiwa kunywa nusu kikombe kutwa mara 3 kwa siku 5 hadi 7.

Dawa hii ni nzuri sana kwa matatizo yote ya mfumo wa uzazi wa mwanamke, Ni dawa ambayo imetumika kwa miongo mingi sana kutibia matatizo mbalimbali ya wanawake. Imethibitika kuwa na uwezo wa:-

(i.) Kusafisha kizazi.

(ii.) Kuzibua Mirija ya Uzazi

(iii.) Inatibu kabisa matatizo ya chango la uzazi

(iv.) Inapevusha haraka mayai hivo kupelekea mwanamke kuwahi kupata mimba.

(v.) Inarekebisha mfumo wa homoni wa mwanamke

(vi.) Inarekebisha mfumo wa hedhi na kutibia maumivu makali wakati wa hedhi.

About the author

Topten Herbs

Topten Herbs ni kituo cha utafiti wa Tiba mbadala zinazoweza kusaidia jamii yetu kujitibia maradhi mbalimbali yanayotukabili kirahisi kabisa kwa kutumia vitu mbalimbali vinavyotuzunguka katika mazingira yetu. Kituo hiki kinapatikana Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

View all posts

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *